Alichokifanya Majizzo kwenye birthday ya Elizabeth Michael ‘Lulu’
Leo April 16,2018 ni siku ya kuzaliwa watu wengi duniani ambao ni maarufu na wengine sio maarufu ila kwa upande wa waigizaji ni siku ya kuzaliwa ya Elizabeth Michael “Lulu” ambaye kwa sasa yupo gerezani akitumikia kifungo chake cha miaka miwili.
Mpenzi wake Elizabeth Michael ambaye ni Majizzo hakutaka siku hii ipite bila kuandika maneno ambayo ni ya muhimu kwa mpenzi wake katika siku hii ya kuzaliwa kwake ingawa yupo gerezani na maneno hayo ameyaandika kupitia ukurasa wake wa instagram.
>>>“Kuna siku yingi zinapita katika maisha ila leo ni siku muhimu, cha kwanza inaelezea kuwa wewe ni mtu muhimu kwenye maisha yako na pili endelea kuwa mtu muhimu kwangu, Nakupenda sana Mama G, Heri ya siku ya kuzaliwa”
Posted