Mtoto wa Cristiano Ronaldo kashaanza kuweka rekodi mapem
Staa wa soka wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Club ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo sasa ni wazi kuwa amepata mrithi sahihi katika kazi yake ya soka Cristiano Ronaldo Junior, Ronaldo JR ameanza kuchukua headlines akiwa bado ana umri wa miaka 7.
Kama hufahamu Cristiano Ronaldo Junior ni mtoto wa kwanza wa Cristiano Ronaldo ana umri wa miaka 7 na sasa ameanza kufuata nyayo za baba yake kwa kuanza kushinda tuzo mbalimbali akiwa bado ana umri wa miaka saba.
Ronaldo Junior April 14 2018 akiwa na bibi yake mzaa baba Dolores Aveiro ameshinda tuzo ya kuwa mfungaji bora wa shule baada ya msimu kumalizika, hiyo ni tuzo ya kwanza ya Ronaldo Junior kupata katika soka na Ronaldo na mama yake wote wamepost katika account zao za instagram kumpongeza Ronaldo Junior.
Posted